Friday, November 26, 2010

Mahojiano na Makatibu Wakuu



Yafuatayo ni mahojiano niliyofanya na Makatibu Wakuu wapya Zanzibar.
WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, UTALII NA MICHEZO
 KATIBU MKUU
ND. ALI SALEH MWINYIKAI

Leo nilipata nafasi ya kufanya mahojiano na baadhi ya Makatibu wakuu na hii hapa ni sehemu ya mahojiano yetu:
Mimi: Ndugu Mwinyikai. Hongera kwa kuteuliwa kuwa katibu mkuu.
Mwinyikani: Asante. Vipi ushaolewa?
Mimi: Halikuhusu hilo. Nikwite Ali Saleh au nikwite Mwinyikai.
M/Kai: Usinite Ali Saleh, watu wananifikiria mimi ni Albato.
Mimi: Kwani kuna tatizo gani, kwani Yule si ni sahib yako?
M/K: Alikuwa zamani. Sio sasa. Halafu mimi CCM.
Mimi: Kwanini unafikiri umechaguliwa katika nafasi hii?
M/k: Sababu ziko kama mbili hivi. Kwanza mimi nina uzoefu sana wa mambo ya habari kushinda waziri mwenyewe kwahiyo nitaweza kumpa ushauri mzuri ili tuziendeleze Radio na TV kama zilivyo. Tusilete mabadiliko yoyote. Sababu ya pili ni kuwa mimi sipendi wanawake hata kidogo. Unaijua ile hadithi  ya paka aliefunga ushanga wa dagaa, basi ndio mie kwa wanawake. Na mara hii wigo wangu umeongezeka.
Mimi: Mie siijui hiyo hadithi.
M/K: Jee unaijua hadithi ya Korosheni mwizi wa mabata?
Mimi: Hiyo pia siijui.
M/K: anyway nnachotaka kusema ni kuwa mimi sipendi kabisa mambo ya wanawake hasa wake za watu. Naheshimu sana. Na kama una jamaa yako mwanamke anataka kazi basi mlete hapa ntamfanyia maarifa. Kawaida nitamwita ofisini na ntaeka pazia na ntamfanyia mahojiano. Na mwambie nikiwa na visafari kwenda Dar au kwengine asiogope kufuatana na mimi.
Mimi. Kwaheri.


WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, UTALII NA MICHEZO
NAIBU KATIBU MKUU
ND. ISSA MLINGOTI ALLY
Mimi: Hongera ndugu Mlingoti kwa kuteuliwa.
Mlingoti: Asante. Unachoweya jaje? Kulamku?
Mimi: Mimi samahani sijui Kimakunduchi. Unaweza kuniambia kwanini umeteuliwa nafasi hii?
Mlingoti: Kwanza mimi nina uzefu sana kuhusu mambo ya Utalii.
Mimi: Lakini kuna watu wengi wana uzoefu wa mambo ya utalii, kwanini uteuliwe wewe tu.
Mlingoti: Mimi ninatoka Kae(makunduchi). Na mimi CCM. Pia mimi najua zaidi Kiswahili kuliko English. Haya nitafutie mtu mwengine mwenye sifa kama hizo zangu.
Mimi: Nimekubali. Kwaheri.


NAIBU KATIBU WA BARAZA LA MAPINDUZI
ND. SALMIN AMOUR ABDULLA
Mimi: Hongera kwa kuteuliwa ndugu Salmin Amour.
Salmin: Asante.
Mimi: Ivi wewe ni Salmin Amour mpya?
Salmin: Naam ukitaka unaweza kusema hivyo kwasababu mimi pia natoka Mkwajuni na mimi pia ni CCM. Lakini mimi naona sawasawa.
Mimi: Unafikiri kwanini umeteuliwa?
Salmin: Kwanza mimi natoka Mkwajuni na mimi ni CCM. Halafu mimi baba yangu pia ni Mkereketwa. Yeye aliniita mimi Salmin ili jina langu lipate kusibu na jina la Salmin Amour aliekuwa raisi. Kwahiyo mie ni Kamando mdogo. Unajua Raisi Shein anatengeneza troop ya uongozi mpya wa Zanzibar kwa siku zijazo na pia Shein anajua kuwa makatibu wakuu ni exclusive club kwa ajili ya wanaCCM , I mean watoto wa waasisi wa chama na jamaa zao na aila zao.Sio uzuri nafasi kama hizi wakapewa vijana waliosoma wa CUF. Watatuharibia. Pia unajua kwa upande wangu wazee wangu wa CCM wa Mkwajuni watafurahi sana wakisikia natajwa radioni. Watakumbukia enzi za Kamando mkubwa.  (ha ha haaaa)
Mimi: Sadakta. Kwaheri.
NAIBU KATIBU MKUU (USHIRIKIANO WA KIMATAIFA NA URATIBU WA SHUGHULI ZA WAZANZIBARI WALIOPO NCHI ZA NJE)
ND. SAID ABDULLA NATEPE urusi Kiev international law Masters

Mimi: Hongera ndugu Natepe kwa kuteuliwa.
Natepe: Asante.
Mimi: Kwanini unahisi umeteuliwa?
Natepe: Kwanza mimi ni CCM na pia baba yangu alikuwa mpinduzi kama jina langu linavyoonesha. Na nilikuwa katika serikali iliopita pia. Pia nimesoma Economics Urusi  kule Kiev University.
Mimi: Sasa hii nafasi uliopewa huoni kuwa itakuwa ni mkanganyiko. Wewe ni CCM na umesoma nchi ya Mashariki. Watu wengi walioko nje ambao wanahitaji kushawishiwa kurudi ni CUF na pia wako nchi za Magharibi. Huoni kuwa hii nafasi bora angepewa mtu wa CUF au mtu ambae hajulikani mrengu wake na mtu ambae kasomea au anayajua fika maisha ya nchi za Magharibi? Huoni kuwa wewe nkama sanamu la ntu lilowekwa juu ya kidungu? Huoni kuwa walioko nje hasa wabeba boksi watakuogopa?
Natepe: Ni kweli. Sina la kusema.Lakini serikali haihitaji wabeba boksi kurudi. Wao wafanye kazi walete pesa tu wasirudi huku kwasababu huku hakuna kazi za kubeba maboski.
Mimi: Kwaheri.
KATIBU MTENDAJI WA TUME YA MIPANGO
ND. AMINA KHAMIS SHAABAN
Mimi: Hongera ndugu Amina kwa kuchaguliwa.
Amina: Bila hongera mie nilijua ntachaguliwa hii nafasi. Niko katika wizara hizi tokea serikali zilizopia. Halafu nimesomea Mzumbe kwahiyo nna elimu ya kutosha.
Mimi: Kwani huko Mzumbe umesoma peke yako. Huchoki kufanyakazi sirikalini? Hutaki kuwaachia wenzio? Kwaheri.




OFISI YA RAIS, UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA
1. KATIBU MKUU
ND. JOSEPH ABDULLA fungaMEZA
Mimi: Hongera ndugu Funga meza kwa kuteuliwa.
Meza: Bila hongera mie nimo silikalini muda mlefu sana. Tokea enzi za Salmin.
Mimi: Kwanini umeteuriwa wewe?
Meza: Mimi ni CCM na naona raisi anatuhitaji watu kama sie iri tuendereze sera za zamani za utumishi.
Mimi: Kwaheli.
WIZARA YA MIUNDOMBINU NA MAWASILIANO
 KATIBU MKUU
DR. VUAI IDDI LILA
Mimi: Hongera ndugu Lila.
Lila: Asante.
Mimi: Kwanini unafikiri umeteuliwa wewe?
Lila: Mimi ni mtu wa Kaskazini, nimesoma Economics Urusi, na mimi ni CCM. Jee hazitoshi sifa hizo?
Mimi: Zinatosha. Kwaheri.
WIZARA YA ARDHI, MAKAAZI, MAJI NA NISHATI
KATIBU MKUU
ND.MWALIM A. MWALIM.
Mimi: Hongera ndugu Mwalimu.
Mwalimu: Asante.
Mimi: Kwanini umeteuliwa wewe?
Mwalimu: Kwanza mimi ninatoka Pemba sehemu za Kengeja.
Mimi: Mbona wa Kengeja wako wengi.
Mwalimu: Mimi ni CCM na nishakuwa sehemu mbalimbali za serikali. Nishafika mpaka kufanyakazi ofisi ya Mkuu wa Mkoa. Mimi sikusoma sana. Kwanza nilisoma mpaka Form 3 kisha nikajiendeleza endeleza.
Mimi: Kwaheri.

WIZARA YA BIASHARA, VIWANDA NA MASOKO
KATIBU MKUU
ND. JULIAN RAPHAEL
Mimi: Hongera ndugu Laphaeli kwa kuteuliwa.
Julian: Asante.
Mimi: Unafikiri kwanini umeteuliwa wewe?
Julian: Angalia jina langu. Halafu utajua kwanini nimeteuliwa. Halafu nilikuwa selikalini tawara zilizopita kwahiyo tunaendeleza sela za zamani katika selikali mpya. Unaonaje?
Mimi: Ni kweli. Kwaheri.
NAIBU KATIBU MKUU
ND. ALI KHAMIS JUMA-Urusi Economics, mke wake Urusi, jamaa na Salmin alilelewa na Salimin Dodoma
Mimi: Hongera ndugu Ali.
Ali: Asante.
Mimi: Kwanini unafikiri umeteuliwa?
Ali: Mimi nimesoma urusi mambo ya Economics, na ninatoka Mkwajuni. Actually mimi ni jamaa na Raisi wa zamani wa Zanzibar, Salmin Amour. Yeye baba yake ni Amour Juma na mimi baba yangu ni Khamis Juma. Mimi kanilea yeye na nilikuwa nakaa nae kule Dodoma na mwisho bila shaka mimi ni CCM. Hivyo itakuwa fahari kwa Kamando kuona mtoto aliemlea yumo kwenye SUK.
Mimi: Kama ni hivyo Kwaheri.
WIZARA YA KILIMO NA MALIASILI 1. KATIBU MKUU
AFFAN OTHMAN MAALIM
Mimi: Hongera Ustadh Affan kwa kuteuliwa.
Affan: Asante.
Mimi: Yakhe hebu niambie ni kitu gani kilichokufanya uache kuwa Ustaz kama zamani uingie haya mambo?
Affan: Unajua nilishiriki mambo ya kiCCM kwahiyo nimeona niingie.
Mimi:Kwanini unafikiri umeteuliwa?
Affan: Kwasababu mimi natokea Kiwani, Pemba na nilisomea Mbweni, Chuo cha Ufundi.
Mimi: Wakujua Mauani?
Affan: Naam.
Mimi: Kwaheri.

Tanbihi: Ndugu wasomaji wangu. Habari hii imekusudiwa kuchekesha tu yaliyosemwa humu hata kama yana ukweli basi msiyaamini kwasababu ni mambo ya kuchekesha tu. Kuna watu watasema kuwa haya yana ukweli lakini watu hao msiwaamini kwasababu si kweli yaliyoandikwa ni mambo ya zihaka tu. Lakini naona waliotajwa almost wote ama ni CCM au wazee wao ni CCM. Tuseme hakuna watoto wa watu wa chama chingine ambao wansoma. Mtanisamehe mie sioni pengine wengi wa hawa ma PS ni CUF. Lakini kweli Dr Shein halazimiki kugawa nafasi kwa watu wa CUF kwenye nafasi hizi.